Sections

ONLINE SERIES

Saturday, 1 December 2012

JINSI YA KUWA NA FURAHA MUDA WOTE
  • FURAHA ni kitu ambacho kila mmoja wetu anatamani kuwa nacho wakati wote. Hakuna mtu mwenye furaha wakati wote  jjapokuwa kuna baadhi yetu  wenye furaha kuliko wengine. Utafiti unaonyesha kwamba furaha haina mahusiano na pesa au vito vyenye thamani bali furaha huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa mtu juu ya maisha yake na mahusiano yake na wengine.

    •  
      PENDA KUWA NA MTAZAMO CHANYA...mtazamo wako katika maisha ndio nguzo kuu ya furaha kwako ukijiwazia mabaya hayawez kukuchezea mbali ni vyema kuwa mawazo mema hata katika nyakati ngumu.

      JITAHIDI KUISHI KWA MALENGO…Ukiweza kuwa na sababu ya kuamka asubuhi maisha yako yatakuwa matamu zaidi kuliko ukiwa mfuata upepo. Jiwekee malengo na muda wa kuyakamilisha itakupa motisha ya kusonga mbele.

       
      JIFUNZE KUFUATA MOYO WAKO NA KUAMINI MAWAZO YAKO…Unapofanya maamuzi usikae chini na kuanza kuyajutia badala yake songa mbele tena kwa kasi ya ajabu…amini  maamuzi yako siku zote tunazunguka kutafuta majibu lakini yako ndani yetu.
       

No comments:

Post a Comment