asubuhi ya leo, hii ni Mandela road kwa wale wanaotaka kuepuka foleni
Monday, 3 December 2012
Saturday, 1 December 2012
JINSI YA KUWA NA FURAHA MUDA WOTE
-
FURAHA ni kitu ambacho kila mmoja wetu anatamani kuwa nacho wakati wote. Hakuna mtu mwenye furaha wakati wote jjapokuwa kuna baadhi yetu wenye furaha kuliko wengine. Utafiti unaonyesha kwamba furaha haina mahusiano na pesa au vito vyenye thamani bali furaha huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa mtu juu ya maisha yake na mahusiano yake na wengine.
-
PENDA KUWA NA MTAZAMO CHANYA...mtazamo wako katika maisha ndio nguzo kuu ya furaha kwako ukijiwazia mabaya hayawez kukuchezea mbali ni vyema kuwa mawazo mema hata katika nyakati ngumu.JITAHIDI KUISHI KWA MALENGO…Ukiweza kuwa na sababu ya kuamka asubuhi maisha yako yatakuwa matamu zaidi kuliko ukiwa mfuata upepo. Jiwekee malengo na muda wa kuyakamilisha itakupa motisha ya kusonga mbele.JIFUNZE KUFUATA MOYO WAKO NA KUAMINI MAWAZO YAKO…Unapofanya maamuzi usikae chini na kuanza kuyajutia badala yake songa mbele tena kwa kasi ya ajabu…amini maamuzi yako siku zote tunazunguka kutafuta majibu lakini yako ndani yetu.
-
Sunday, 11 November 2012
Dalili 6 za "looser boyfriend"
1. Hana mwelekeo wowote juu ya maisha ya baadae.huyu ni kiumbe ambaye yupo yupo tu humu duniani,anakuwa msindikizaji,hana mpango maalum wa kuboresha maisha yake na wala hakereketwi na hali yake ya sasa, si mtu mzuri kuambatana nae, atakupotezea muda na kukurudisha nyuma kimaendeleo, ladies watch out.
2. Haoni tabu kushinda ndani siku nzima bila shughuli ya kufanya.
kiumbe huyu haoni tabu kukaa ndani na kumwacha mkewe awe "breadwinner" wakati ni jambo la aibu kwa mwanaume kukaa na kupokea kwa mkewe lakini yeye atakuuliza tunakula nini leo bila kujua pesa ya chakula inakotoka
3. Kama aliwahi kuzaa kabla hujamjua na hana muda na watoto au mtoto wake
wanawake wengi hudhani kwamba baba akiwa hana muda na mtoto wa mwenzie basi yeye ndio anayependwa sana lakini uhalisia ni kwamba mwanaume asiyejali watoto wake si mtu bora na ni bora kujiepusha nae mapema
4. Hana muda na wala havutiwi na mafanikio yako binafsi.
mara nyingi kiumbe huyu hana muda na mafanikio yako wala hatambui ndoto zako na hana ushauri wa kukujenga.
5. Hana muda na usafi wake binafsi.
somehow, somewhere unaweza kukuta hajijali kimavazi na hata kiusafi huweza kukutia aibu mbele ya rafiki na nduguzo
6. Hawezi kusimama kwa miguu yake mwili, hutegemea ndugu na familia
yeye kila siku ni kukopa, mara leo kwa baba, kesho kwa kaka, kesho kutwa kwa rafiki zake anakutia aibu sababu hataki kuishi ndani ya uwezo wake
Subscribe to:
Comments (Atom)






