Sections

ONLINE SERIES

Sunday, 11 November 2012


Dalili 6 za "looser boyfriend"
1. Hana mwelekeo wowote juu ya maisha ya baadae.
    huyu ni kiumbe ambaye yupo yupo tu humu duniani,anakuwa msindikizaji,hana mpango maalum wa  kuboresha maisha yake na wala hakereketwi na hali  yake ya sasa, si mtu mzuri kuambatana nae, atakupotezea muda na kukurudisha nyuma kimaendeleo, ladies watch out.
2. Haoni tabu kushinda ndani siku nzima bila shughuli ya kufanya.
   kiumbe huyu haoni tabu kukaa ndani na kumwacha mkewe awe "breadwinner" wakati ni jambo la aibu kwa mwanaume kukaa na kupokea kwa mkewe lakini yeye atakuuliza tunakula nini leo bila kujua pesa ya chakula inakotoka
  
3. Kama aliwahi kuzaa kabla hujamjua na hana muda na watoto au mtoto wake
    wanawake wengi hudhani kwamba baba akiwa hana muda na mtoto wa      mwenzie basi yeye ndio anayependwa sana lakini uhalisia ni kwamba mwanaume asiyejali watoto wake si mtu bora na ni bora kujiepusha nae mapema
4. Hana muda na wala havutiwi na mafanikio yako binafsi.
    mara nyingi kiumbe huyu hana muda na mafanikio yako wala hatambui ndoto zako na hana ushauri wa kukujenga.
5. Hana muda na usafi wake binafsi.
    somehow, somewhere unaweza kukuta hajijali kimavazi na hata kiusafi huweza kukutia aibu mbele ya rafiki na nduguzo
6. Hawezi kusimama kwa miguu yake mwili, hutegemea ndugu na familia
    yeye kila siku ni kukopa, mara leo kwa baba, kesho kwa kaka, kesho kutwa kwa rafiki zake anakutia aibu sababu hataki kuishi ndani ya uwezo wake


No comments:

Post a Comment